Bodi ya Nne ya Uendeshaji ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD), leo Agosti 7, 2026 imeanza rasmi kutekeleza majukumu yake baada ya kuapishwa na kufanya kikao chake cha kwanza.
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Dkt. Rosemarie Mwaipopo, Kampasi Kuu ya Tengeru, kiliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. John Elton Lusingu.
Kikao kimehudhuriwa na Katibu wa Bodi ambaye ni Mkuu wa Chuo, Prof. Bakari George, pamoja na wajumbe Dkt. Waheeda Shokat, Dkt. Alex Nkondola, Bw. Yasin Sanuku, Bw. Bahati Ndoweka na Bw. Martin Mashaka.
Awali kabla ya kuanza kwa kikao hicho wajumbe wa Bodi waliapishwa na kamishna wa viapo, Wakili Dunstan Shimbo ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria - TICD.
Kuapishwa na kuanza kwa shughuli za Bodi hiyo kunaiweka TICD katika nafasi mpya ya kuimarisha usimamizi wa kimkakati, kuongeza ubora wa elimu na mafunzo, kuimarisha tafiti na ubunifu.
Kupitia uongozi wa Bodi hiyo mpya, TICD inatarajia kuharakisha utekelezaji wa vipaumbele vya maendeleo ya Chuo, kuongeza ushindani wa kitaaluma na kuendelea kujijengea nafasi kama kitovu cha umahiri katika elimu ya maendeleo ya jamii nchini na kanda ya Afrika Mashariki na Kati.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mameneja kampasi kutoka kampasi zote nane za Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru
Published: 22 Aug 2026