Waitaja TICD Kuwa Jicho la Meru DC, Arumeru
Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) kimetajwa kuwa jicho na Taasisi ya kutegemewa na kutumainiwa na serikali katika wilaya ya Arumeru na Halmashauri ya Meru.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Mwinyi Ahmed Mwinyi, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mwl. Zainab Makwinya, wameisifu hadharani TICD,
leo tarehe 8 Julai, 2026 wakati wa Kongamano la Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Meru lililofanyika katika chuoni TICD, wakisisitiza kuwa mchango wa chuo hicho katika maendeleo ya vijana, jamii na Taifa umeifanya TICD kuwa taasisi ya kimkakati inayostahili kuungwa mkono na kuthaminiwa.
Kongamano hilo, lililobebwa na kaulimbiu "Vijana Tuyajenge, Tanzania ni Yetu," limewakutanisha mamia ya vijana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Meru, wakiwemo wanafunzi wa TICD, linafanyika kwa lengo la kuhamasisha uzalendo, ushiriki wa vijana katika maendeleo na maandalizi ya mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru tarehe 11 Julai, 2026.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Chuo, Dkt. Juma Almasi Mhina ameushukuru uongozi wa Wilaya ya Arumeru na Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa imani kubwa wanayoionesha kwa TICD, akiahidi kuwa chuo hicho kitaendelea kuwa mshirika wa karibu katika kutekeleza agenda za maendeleo ya jamii, kuwawezesha vijana na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kujenga Taifa lenye ustawi.
Jackson Mhoho na Glory Mlay ni miongoni mwa wahadhiri wa TICD wawezesha mada katika kongamano hilo.
Published: 22 Aug 2026